Wednesday, May 9, 2012
09 MARCH.HII NDIO PESA ILIYOCHANGWA KWA AJILI YA KUMTIBU SAJUKI
Baada ya watanzania kujitolea pesa za kwenda kumtibu India mwigizaji Sajuki, hatimae kiasi kilichochangwa na siku ya safari vyajulikana.
Wastara ambae ni Mke wa Sajuki, amesema imefikia hatua ambayo ni nzuri na wanaweza kuondoka kwenda India japo pesa haijafikia yote.
Pesa iliyokua inatakiwa ni milioni 25 lakini iliyopatikana ni milioni 16 lakini tayari itawawezesha kusafiri kwenda India jumapili au jumatatu ijayo kwa sababu pesa nyingine bado zinaendelea kukusanywa.
Wataondoka yeye, Sajuki pamoja na kaka wa Sajuki na watakaa India kwa wiki mbili lakini kama kutakua na mabadiliko yeyote atasema na millardayo.com
Mwishoni mwa wiki iliyopita Wastara alithibitisha kuibiwa zaidi ya laki nane kwenye account ya pesa ya simu yake ya mkononi baada ya wajanja wa teknolojia kuzuia pesa zilizokua zinatumwa na watanzania kwenye simu yake, na walifanikiwa pia kuiba pesa zilizokuwemo kwenye account ya Wastara.
SOURCE. www.jojothefigher.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment