tuwasiliane

Tuesday, January 10, 2012

10 JAN.9 AZAM YAENDELEZA UBABE KWA VIGOGO: YAITANDIKA SIMBA 2-0 NA KUIVUA UBINGWA



Timu ya Azam FC imekuwa zaidi ya shule kwa timu za Simba na Yanga katika michuano ya Mapinduzi Cup, kufuatia kuifundisha Yanga kucheza mpira na kisha kuwapa somo Simba kutumia nafasi wanazopata.

Washambuliaji wawili wasio kubalika nchini Gaudence Mwaikimba na John Raphael Bocco ndio waliopeleka kilio kwa Simba hii leo, ambapo Simba walitengeneza nafasi za kutosha na kushindwa kuzitumia.

Mchezo ulitulia kati huku viungo wa Simba wakitawala eneo hilo katika kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi lukuki ambazo ziliishia kupotea huku Azam FC wakitumia vyema nafasi ya dakika 10 kujipatia goli la kuongoza lililo fungwa na John Raphael Bocco.

Simba ambao walionekana kuwa nadhamira ya kusawazisha goli hilo bila mafanikio, walipigiwa msumari wa pili na mtokea bench Gaudence Mwaikimba aliyechukua nafasi ya Kipre Tchetche katika dakika ya 85 na katika dakika ya 90 alitupia goli la pili.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Amani Zanzibar ulishuhudiwa na mashabiki lukuki, huku mchezo ukiwa ni wakasi na ushindani Mkubwa.

Kwa matokeo hayo ya goli 2-0 walio upata Azam FC, una wavua ubingwa Simba na hivyo Azam kutinga fainali ambayo itachezwa january 12 katika uwanja wa Amani, wakati mpinzani wake akitarajiwa kujulikana Kesho pale Mafunzo watakapo chuana na Jamhuri ya Pemba katika nusu fainali ya pili.

No comments:

Post a Comment