Sunday, January 8, 2012
08 JAN. Pambano litarudiwa
Chama cha ndondi duniani ' World Boxing Association' kimeamuru pambano kati ya Amir Khan na Lamont Peterson lirudiwe bila kupoteza wakati, kwa mujibu wa ma promota wa Khan.
Khan alipoteza mataji yake mawili la WBA na IBF kwa Lamont Peterson mwezi disemba lakini akahoji masuala kadhaa yaliyotokea wakati pambano hili likiendelea.
Moja ya madai ni kwamba kuna mtu mmoja ambaye hakutambulika, na sasa amefahamika ni nani, aliyeonekana kuingilia shughuli za mwamuzi mmoja wa WBA.
"kutokana na hilo sasa WBA...itaamuru pambano hilo lirudiwe, amesema Mkurugenzi wa kampuni ya Golden Boy Promotions, Richard Schaefer.
Mkuu huyo amesema kua "tumepokea risala ikithibitisha habari hizo mapema leo jumamosi na ujumbe wa mandishi utatufikia jumanne ijayo.
"hiyo ina maana kua wapiganaji hawa wawili hawawezi kushiriki pambano lolote kabla ya pambano la marudiano. Hivyo ndoto za Peterson ya kutaka apambane na mtu mwingine kujizidishia kipato na sifa zimefifia.
Mkurugenzi wa Golden Boys anasema wanataraji Chama cha IBF nacho kitakubaliana na uwamuzi wa WBA.
Hapo awali, Rais wa WBA Gilberto Mendoza ameiambia BBC michezo kua, hali hii inazua mizengwe na hivyo inabidi pambano lirudiwe kuondoa mashaka.
Halimashauri ya ndondi ya Washington imelaumiwa kwa kutofuata utaratibu unaostahiki pambano kama hilo.
Khan alipoteza pambano hilo la uzani wa light-welterweight kwa pointi chache baada ya kupokonywa pointi zake mbili kwa kumsukuma mpinzani wake.
Amir Khan na taji moja
Majaji George Hill na Valerie Dorsett waliamua pambano hilo 113 kwa 112 kwa Peterson, huku Jaji mwingine Nelson Vasquez akimpa Khan ushindi wa 115-110.
Kwa mujibu wa maandishi ya kadi ya Hill imeonekana kua uwamuzi wake wa awali Khan alishinda raundi ya saba lakini baadaye alibadili uwamuzi na kumpunguzia Khan pointi na hivyo Peterson kupata ushindi wa 10-8, jambo ambalo bila mabadiliko ya baadaye ya Jaji Hill Khan angeibuka mshindi wa pambano
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment