tuwasiliane

Tuesday, February 14, 2012

14 FEB.LINAH ASEMA LICHA YA KUOKOKA HATAACHA BONGO FLAVA


Msanii mwanadada mrembo ambaye ina aminika amezima nyota za wasanii wengi wa kike tangu aingie rasmi kwenye muziki, namzungumzia Estalina Sanga ‘Linah’, ameweka wazi kuwa pamoja na yeye kulelewa katika mazingira ya kidini lakini haoni kama atakuja kuacha kuimba nyimbo za kawaida (za Kidunia) kwani ndio kipaji chake.

Linah ambaye awali alikuwa akiimba kwaya lakini katika kutafuta maisha akaamua kukimbilia muziki huo wa kidunia kwa ajili ya kutafuta maslahi ambao umeweza kumpa jina kubwa katika ukanda huu wa afrika mashariki.

Kwa mujibu wa mwanadada huyo, kikubwa ambacho wazazi wake wamekuwa wakimsisitizia kila siku ni juu ya kulinda heshima yake ya familia pamoja na kuachana na tabia chafu ambazo zinaweza kuchafua jina la familia yao.

Alisema kuwa hata katika upande wa mavazi ya utata ambayo amekuwa kivaa akiwa kwenye stage huwa havai muda wote kwani anaheshimu busara za wazazi ambao ndiyo nguzo kubwa katika maisha yake.

No comments:

Post a Comment