tuwasiliane

Friday, August 11, 2017

Tshishimbi Wa Yanga Kutua Rasmi Kesho

 -Kiungo mpya mkabaji wa klabu ya Yanga kutoka DRC Congo, Papy Kabamba Tshishimbi anatarajiwa kuwasili nchini kesho kwa ajili ya kujiunga rasmi na kambi ya timu hiyo.
Awali kulikuwa na taarifa ambazo zinadai kuwa kiungo huyo angewasili leo lakini badala yake kumekuwa na mabadiliko ambayo yatamfanya awasili kesho badala ya leo.
Akiongea na chanzo chetu, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika amesema Tshishimbi alitakiwa ajiunge na timu tangu wiki hii ilipoanza lakini hati yake ya kusafiria (pasipoti) ndiyo ilikwamisha.
“Tshishimbi anaingia kesho sio leo. Kulikuwa na tatizo kidogo kwenye tiketi yake kutokana na wakala kushindwa kumpelekea tiketi mapema kwahiyo ndege ilikuwa imejaa hivyo ataingia kesho”, alisema.
Nyika aliongeza kuwa nyota huyo hataweza kucheza mchezo dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa kesho ingawa ataushuhudia mchezo huo kutokea jukwaani.
“Mechi dhidi ya Ruvu Shooting ataweza kuiona kwani ataingia asubuhi au mchana lakini pia hata kama angekuja leo asingeweza kucheza kesho ila ataongozana na wenzake kwenda kwenye kambi ya visiwani Zanzibar”, alisisitiza Tshishimbi
Awali Tshishimbi alitua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa ligi Kuu soka Tanzania bara kabla ya kurejea nchini kwao kwa ajili ya masuala ya kifamilia ambapo kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina alisema kuwa kiungo huyo ni bora na anakuja kutibu tatizo la kiungo mkabaji ambalo limekuwa likiikumba klabu hiyo kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment