tuwasiliane

Sunday, August 13, 2017

JULIO AKUBALI MATOKEO BAADA YA KUANGUKIA PUA

Kocha Jamhri Kihwelu ‘Julio’ amepigwa chini kwenye uchaguzi wa TFF baada ya kuambulia kura mbili (2) katika kinyang’anyiro cha ujumbe wa kamati ya utendaji ambapo alikuwa anagombea kupitia Kanda ya Dar es Salaam ambayo ilikuwa na jumla ya wagombea 12 huku akitakiwa mjumbe mmoja tu kati yao.
Baada ya kuanguka vibaya, Julio amesema ameridhika na amekubali matokeo ambayo yamepatikana kutoka na uchaguzi uliokuwa wa wazi, haki na Democrasia.
“Nimeridhika na matokeo, waliochaguliwa wamechaguliwa kwa haki, uchaguzi ulikuwa wa wazi na haki. Uchaguzi huu umekwenda vizuri kwa sababu TAKUKURU wamesimama kidete tangu mwazo, namshukuru mkurugenzi wa TAKUKURU na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hiyo ndio sera yake ya uwazi na ukweli. Na kama tutaenda hivi itafika hata kwenye ligi timu zinasajilitushindane uwezo sio timu inakuja kupata ushindi mezani au kwakuwa ilitayarishwa lazima ishinde.”
“Waliochaguliwa wasilete urafiki kwamba huyu alinisaidia kwenye uchaguzi, wawaweke watu ambao wanauwezo wa kufanya kazi ili tuendelee. Tumechoka kuwa na nyimbo kila siku AFCON, CHAN, World Cup na tunashindwa kwenda kwa sababu hatuna misi bora.”
“Sisi tulioshindwa ni familia ya mpira, tutakaa na viongozi waliochaguliwa tuwape maoni yetu tuwaeleze kitu gani cha kufanya na nina hakika kabisa watakuwa wasikivu. Mimi kama Julio sio lazima kuchaguliwa kuwa kiongozi lakini kama kuna mtu atafanya kile ambacho na mimi nakihitaji basi sina shaka. “
“Viongozi waliochaguliwa nawaunga mkono kwa 100% na sisemi hivi kwa kuwa nataka ch ochote kwa sababu viongozi wamepatikana kwenye misingi bora naendelea kuwashukuru TAKUKURU kwa kazi waliyoifanya.”

No comments:

Post a Comment