tuwasiliane

Sunday, May 20, 2012

20 MAY. CHELSEA BINGWA WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

WASWAHILI HUSEMA MPIRA NI DAKIKA 90 HALI AMBAYO IMEJIDHIHIRISHA LEO BAADA YA TIMU YA CHELSEA YA UINGERZA KUWEZA KUNYAKUWA KOMBE LA CHAMPIONS LEAGUE. WACHAMBUZI WENGI WA SOKA WALIKUWA HAWAIPI KIPAUMBELE CHELSEA KABISA KUCHUKUA KOMBE LA CHAMPIONS LEAGUE MBELE YA BAYERN MUNICH NYUMBANI KWAO, KWNYE DIMBA LA ALLIENCE ARENA.

KATIKA MECHI HIYO AMBAYO BINGWA ALIPATUKANA KWA NJIA YA MATUTA BAADA YA KUTOKA KATIKA DK 120 WAKIWA SARE YA GOLI 1-1. ILIKUWA NI BAYERN MUNICH ILIYOPATA GOLI LA KUTANGULIA KATIKA DAKIKA YA 83 KUPITIA KWA THOMAS MULLER, DAKIKA TANO BAADAE DIDIER DROGBER ALIWAINUWA WASHABIKI WA CHELSEA KWA KUSAWAZISHA GOLI KWA KUUNGANISHA KLOSI SAFI KAWA KICHWA.HADI DAKIKA 90 ZINA MALIZIKA MATOKEO YALIKUWA 1-1

DAKIKA 30 ZILIONGEZWA, AMBAPO BAYERN MUNICH WALIKOSA PENATI KATIKA DAKIKA YA 5 YA KIPINDI CHA KWANZA CHA DAKIKA ZA NYONGEZA BAADA YA DROGBA KUMKATA FRANK RIBBERY, AMBAPO MSHAMBULIAJI WA BAYERN ROBEN ALIWEZA KUKOSA PENATI HIYO BAADA YA KIPA KUDAKA.
HADI DAKIKA 120 ZINAMALIZIKA MAGOLI YAKABAKI 1-1. NDIPO PENATI ZIKAPIGWA AMBAPO CHELSEA WALIPATA PENATI 4 NA BAYERN WALIPATA PENATI 3.

HIVYO NI KWA MARA YA KWANZA KWA TIMU YA CHELSEA KUWEZA KUCHUKUA KOMBE LA CHAMPIONS LEAGUE. PIA ITAUKWA NAFASI KWA MMILIKI WA CHELSEA KUWEZA KUMPA MKATABA WA KUWA KOCHA MKUU,KOCHA ANAYEKAIMU UKOCHA MKUU KWA SAA MUITALIANO DI MATEO

No comments:

Post a Comment