tuwasiliane

Wednesday, May 16, 2012

16 MAY.Yeye ya Jaydee yasheheni lugha nne


Ni msanii mwenye mafanikio makubwa kwenye sanaa ya Muziki huo, kwani ameweza kugusa wengi kwenye kibao hicho ambacho ameimba kwa kutumia lugha mbalimbali kikiwemo Kiswahili, Kiingereza,Kilingala na Kiganda.

Alisema kwamba ameamua kutumua lugha hizo tofauti ili kuwakilisha mashabiki wa maeneo mengine, ambao wamekuwa wakifurahia kazi zake huku wakitatizwa na lugha.

Si mwingine bali ni yule Nguli wa Muziki wa Bongo Flava hapa nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee', amefyatua tena mpini wake mpya uliokwenda kwa jina la 'Yeye' uliotumia lugha nne.

Kwani mpini huo ameupika ndani ya Studia ya Fish Crab za hapa Jijini, chini ya mtayarishaji Lamar na imeshaanza kufanya vema kwenye vituo mbalimbali vya redio na kuteka nyoyo za mashabiki.

Ni mara nyingine tena kwa mwanadada huyo kufyatua Singo iliyosheheni lugha tofauti, kwani hapo awali aliwahi kuachia Distance, Mimi ni Mimi alioimba na Oliver Mtukudzi na nyinginezo zikiwa katika lugha zaidi ya moja.
Images:

No comments:

Post a Comment