tuwasiliane

Monday, May 14, 2012

14 MAY.Mbunge anusurika kutandikwa Mapanga!


Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), amenusurika kucharangwa mapanga, baada ya kundi la vijana wanaoaminika kuwa wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumvamia baada ya kukerwa na hatua ya kuhama kwa karibu uongozi mzima wa chama hicho Kata ya Nduli.



Kundi hilo lilimvamia Msigwa alipokuwa akijiandaa kuondoka akiwa na viongozi wanane waliokuwa wa CCM wa kata hiyo, ambao walihamia CHADEMA jana, ambapo walianza kuwashambulia watu walioandamana naye na kuwajeruhi vibaya kwa mapanga watu wawili, kiasi cha kulazimika kukimbizwa hospitalini kwa matibabu.



Hata tetesi zimedai kuwa kundi hilo la vijana lilitumwa na mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho, kwa madai ya kukasirishwa na hatua ya kuhama kwa mwenyekiti, katibu na wajumbe sita wa CCM Kata ya Nduli, ambao waliwaongoza zaidi ya wanachama 90 kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA.
SOURCE; DARHOTWIRE

No comments:

Post a Comment