tuwasiliane

Friday, January 6, 2012

06 JAN.BREAKIN NEWS,KUMBE IRENE UWOYA KAPINDULIWA NA SHOGA YAKE


MAKUBWA! Irene Uwoya aliyeimbwa na Naseeb Abdul ‘Diamond’ kwenye ngoma ya Nimpende Nani kuwa, ni mchaga mwenye hasira, ameangua kilio laivu kwa shoga’ake, Janeth Mathias, akidai ndiye chanzo cha kuparanganyika kwa ndoa yake na Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
Katika hali ya kushangaza, wakati Ndikumana akitangaza kutema ndoa yake rasmi na mrembo huyo, nyuma ya pazia kuna ishu nzito, The Udaku Master, Ijumaa lina ‘eksiklusivu’.
UWOYA ATIKISWA
Kwa mara ya kwanza, Uwoya ambaye ni mwanamke wa shoka asiyetishika, amekiri kutikiswa na Janeth ambaye ni rafiki yake kipenzi.
LAZIMA MANENO YAMTOKE
Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam juzi, Uwoya au mama Krish ambaye ni moto wa kuotea mbali katika muvi za Kibongo, alisema mbali na kumshuhudia Janeth akiwa kwenye malavidavi na mumewe, lakini pia amekuwa akitonywa juu ya ishu hiyo na watu wake wa karibu.
FULU HASIRA
Huku akionekana mwenye hasira, Uwoya alisema: “Walahi Janeth ni rafiki yangu tangu tukiwa sekondari, mwanzoni niliona ni kawaida tu kwa mtu na shemeji yake kuwa ‘klozi’, lakini sikuamini macho yangu nilipowashuhudia laivu ‘waki-kisi’.
“Simsingizii Janeth, nina ushahidi wa kutosha kuwa ndiye aliyepindua ndoa yangu.
“Hapa nina hasira naye, wee acha tu.”
Ijumaa: Kwani Ndikumana ‘ku-kisi’ ni tatizo?
Uwoya: Si tatizo ila najaribu kutumia maneno ya kistaarabu. Niliumia sana, nimeamini kikulacho ki nguoni mwako.
Ijumaa: Ulipomuuliza Ndikumana alisemaje?
Uwoya: Aseme nini? Kwani kulikuwa na haja ya kuuliza huku kila kitu kipo wazi? Unaambiwa kama kusoma hujui, hata kuangalia picha hujui?
Ijumaa: Hiyo ishu ilitokea wapi?
Uwoya: Ishu nzima ilitokea siku ya birthday yangu Tangi Bovu (Dar).
Ijumaa: Unaweza kufafanua ilikuwaje?
Uwoya: Huwa sitaki kukumbuka lile tukio kwani moyo unauma sana, ieleweke nina ushahidi wa kutosha na sibahatishi.
Ijumaa: Baada ya kugundua umepinduliwa ulimwambia nini rafiki yako Janeth?
Uwoya: Kwanza nilimshukuru kwa kunigeuka na kunivurugia ndoa yangu. Tafadhali naomba niishie hapo, lakini habari ndiyo hiyo, mwizi wa mume wangu ni yeye.

JANETH MWENYEWE HUYU HAPA
Baada ya kusikia kilio cha Uwoya, Ijumaa lilimsaka kwa udi na uvumba mwanamke ‘aliyeshushiwa jumba bovu’ na staa huyo ambapo alipopatikana alisomewa msala ‘eituzedi’.
Huku naye akiwa ‘amepaniki’ vibaya, alifunguka: “Kwanza Irene (Uwoya), aache kutafuta visingizio kwani ndoa ilimshinda siku nyingi.
“Ni kweli Irene ni rafiki yangu wa siku nyingi, mimi ni mke wa mtu, siwezi kumpindua kwenye ndoa yake, zaidi sana namuonea huruma.

NI KWELI NDIKUMANA ALINISIFIA
“Kwenye birthday yake, ni kweli nilikaa na Ndikumana meza moja na ni kweli alinisifia na nilimshirikisha kila mtu.

VITISHO
“Cha ajabu, badala Irene aungane na mimi tumkemee Ndikumana, akaanza kunitumia vitisho kwamba nimevunja ndoa yake.

MENGI YAIBUKA
“Irene nimeshamstiri sana kwani amekuwa akimpigia simu mume wangu, lakini mimi sikumuuliza.

SIJAMVULIA NDIKUMANA
“Uwoya anatakiwa kuamini kuwa sijawahi kumvulia nguo Ndikumana na haitatokea.

NDIKUMANA ANAJIPANGA
Alipotafutwa Ndikumana kusema anachokijua juu ya timbwili hilo alisema: “Bado najipanga kupasua jipu kuhusu Irene.”

HISTORIA
Ndikumana alimuona Uwoya kwenye muvi ya Oprah ambapo ghafla moyo wake ‘ulimdondokea’ na kufanya taratibu za kumpata ndipo wakafunga ndoa ya kifahari iliyotafuna takribani Sh. milioni 80, Julai 11, 2009 katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na kufuatiwa na sherehe ya kufa mtu kwenye Hoteli ya Giraffe View Mbezi Kawe, Dar.
Kwa mujibu wa Ndikumana, ndoa hiyo imevunjika rasmi. Ili kujua alichokisema Ndikumana kuhusu sababu ya kuvunja ndoa hiyo, usikose magazeti yajayo ya Global.


SOURCE GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment