SIMBA LEO IMEWEZA KUCHUKUWA UBINGWA KWA SHANGWE YA AINA YAKE BAADA YA KUWEZA KUIFUNGA YANGA GOLI 5-0 KATIKA MCHEZO ULIOFANYIKA KATIKA UWANJA WA TAIFA
ILIWACHUKUA SIMBA DAKIKA MOJA TU TANGU KUANZA KWA MPIRA AMBAPO EMANUEL OKWI ALIWEZA KUTIA MPIRA KWENYE KAMBA NA KUANDIKA GOLI LA KWANZA. GOLI HILO LILIWEZA KUDUMU HADI KIPINDI CHA KWANZA KINAMALIZIKA;
KIPINDI CHA PILI KILIANZA KWA KASI AMBAPO DAKIKA YA 55 SIMBA ILIPATA PENATI BAADA YA EMANUEL OKWI KUFANYIWA MADHAMBI AMBAPO FELIX SUNZU AITIA MPIRA KWENYE KAMBA NA KUANDIKA GOLI LA PILI
EMANUEL OKWI ALIWEZA TENA KUIANDIKIA SIMBA GOLI LA TATU KATKA DAKIKA YA 63 BAADA YA MABEKI WA YANGA KUZEMBEA.DAKIKA YA 70 JUMA KASEJA ANAIANDIKIA SIMBA GOLI LA NNE KWA NJIA YA PENATI BAADA YA OKWI KUANGUSHWA TENA KATIKA ENEO LA HATARI.DAKIKA YA 75 CHUJI ANAMPIGA TENA KWANJA KWA MAKUSUDI EMANUEL OKWI NA PATRICK MAFISANGO ANAWEKA MPIRA KATIKA KIMIA NA KUANDIKA GOLI LA 5 HADI MWISHO WA MCHEZO SIMBA 5 YANGA O. SIMBA WAMEWEZA KUKABIDHIWA KOMBE LA USHINDI WA LIGI KUU
No comments:
Post a Comment