
Wekundu wa Msimbazi Simba SC wametoshana nguvu ya goli 1-1 na Tusker ya Kenya, katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo vinara wa ligi kuu ya vodacom, Simba walikuwa wa Mwanzo kupata goli katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Patrick Mutesa Mafisango kwa mkwaju wa penati.
Mabingwa wa Kenya Tusker walisawazisha goli hilo katika kipindi cha pili na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
Mchezo huo wa kirafiki ulikuwa maalum kwa ajili ya maandalizi ya kombe la shirikisho dhidi ya Kiyovu ya Rwanda, na Ligi kuu ya Vodacom kwa upande wa Simba. Na klabu bingwa Afrika pamoja na Ligi kuu ya Kenya kwa upande wa Tusker.
No comments:
Post a Comment